WANANCHI Wilayani Tarime mkoani Mara,wameombwa kutumia
misimu miwili ya mvua katika wilaya hiyo kulima mazao mbalimbali yakiwemo
ya biashara kwa ajili ya kupambana na umasikini.
Afisa kilimo wa Wilaya ya Tarime Bw Selvanus Gwiboha,amesema
wilaya ya Tarime ina uhakika wa kulima na kuvuna chakula kwa
mwaka kutokana na kuwa ardhi yenye rutuba ya kutosha lakini wananchi wake
hawaitumia kwaajili ya kuongeza uzalishaji mazao ya kchakula na biashara.
Amesema katika msimu huu wa masika Wilaya hiyo
inatarajia kuvuna tani 180,106 ambacho kitatosha na kubaki hadi msimu wa
vuli utakaoanza Septemba 2012 hadi Januari 2013.
Amesema wilayani hiyo ina eneo linalofaa kwa kilimo ni
la zaidi hekta 790,630 ambapo eneo linalolimwa ni hekta 69,155 sawa na asilimia
76.30 eneo linalofaa kwa kilimo.
Hata hivyo afisa kilimo huyo amesema wilaya imepokeaji
na kusambazaji wa vocha za pembejeo jumla za bilioni 1.296 kwaajili ya tani
18,000 za kutosheleza wakulima 18,000 sawa na ekari 18,000,mbolea tani
18,000,Urea tani 18,000 na mahindi chotara tani 18,000 pia jumla ya vijiji 89
vimenufaika na ruzuku za pembe jeo.