BUNDA
MWANAMKE mmoja Bi Sarah Abidenego mkazi wa mtaa wa
Chiringe katika mamlaka ya mji mdogo wa Bunda mkoani Mara,amejifungua
mtoto akiwa na vichwa viwili.
Akizungumza katika wodi ya wazazi katika
hosptali ya teule ya DDH iliyoko mjini Bunda mama huyo amesema kuwa
alipokuwa mjamzito alikuwa akisumbuliwa sana na maumivu ya mgongo na kwamba
ilipofika siku ya kujifungua juzi julai 24 alikwenda katika hosptali hiyo
kwa ajili ya kujifungua.
Amesema baada ya kufika hospitalini hapo
alipokelewa na kupelekwa katika wodi ya wazazi na kwamba ilipofika majira
ya 3.45 abuhi alijifungua mtoto huyo ambaye alikuwa na jinsi ya
kike huku akiwa na vichwa viwili.
Akielezea suala hilo muuguzi wa zamu katika wodi hiyo
,Bi Sophaleti Majanjala,amesema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa
kilo 1.9 na kwamba baada ya kuzaliwa alikaa muda wa saa moja
na baadaye alifariki dunia.
Hata hivyo mama huyo amemshukuru mungu kwa kuwa ndiye
aliyempa kiumbe hicho na pia ndiye aliyekichukuwa kwa hivyo ana matumaini
kuwa iko siku atabeba mimba na atazaa mtoto aliye na viungo kamili kwani hiyo
ni mimba yake ya kwanza.