BUNDA
Serikali wilayani
Bunda mkoani Mara imewataka watumishi wa
wilayani humo watakaoshindwa kutekeleza kazi za Serikali kuacha kazi kwa
hiari
kabla hawajachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kauli hiyo
imetolewa na mkuu wa wilaya hiyo Bw Joshua Mirumbe katika mkutano wa
hadahara katika
kijiji cha Nansimo katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha kwa
wananchi wilayani humo.
Katika mkutano huo
mkuu wa wilaya huyo alimewaeleza wananchi kuwa mipango mingi ya Serikali
haifanikiwi kutokana na baadhi ya maofisa kukaa maofisini na kushindwa
kwenda
vijijini jambo linalosababisha wananchi kukata tamaa na kuongezeka kwa
umaskini.
Mkuu huyo wa wilaya
ametumia nafasi hiyo kuwaonya watumishi wote wilayani humo na kamwe
hatowavumilia watumishi watakaoshindwa
kutimiza wajibu wao.
Mbali na kutoa
angalizo hilo kwa watumishi wa serikali wilayani humo,Mkuu huyo wa
wilaya
amewataka wazazi kuwasomesha watoto wao ili taifa lipate wataalam wengi
wa fani
mbalimbali.
Na Augustine Mgendi