Mh Vincent Nyerere akiwa Victoria fm ( Picha na Maktaba)
Taarifa zinasema Meli hiyo imezama katika eneo la Chumbe jirani na Zanzibar
Kwa mujibu wa Mbunge wa jimbo la Musoma Mjini Mh Vincent Nyerere akiwa Visiwani Zanzibar amesema kuwa mpaka sasa idadi kamili ya watu waliopoteza Maisha kutokana na ajali ya Meli ya Sea star bado haijafahamika.
Mh Nyerere akiongea na kituo cha redio cha Victoria Fm cha Mjini Musoma amesema kuwa kwa mujibu wa watu waliokuwa katika meli hiyo wamesema kuwa Meli hiyo ilikuwa imebeba watu zaidi ya wale wanaotakiwa
Mbunge huyo amesema kuwa mpaka kufikia jioni tayari watu waliokolewa walikuwa 149 huku maiti ambazo tayari zilikuwa zimepatikana zilikuwa 29.
Ameongeza kuwa kazi za uokoaji zilikuwa ngumu na hivyo kuhairisha kazi hiyo mpaka kesho huku akisema kuwa tayari Meli hiyo imezama kabisa