WATU ZAIDI YA 200 WAHOFIWA KUFA MAJI KUTOKANA NA KUZAMA KWA MELI

           Mh Vincent Nyerere akiwa Victoria fm  ( Picha na Maktaba)

Kwa mujibu wa Mbunge wa jimbo la Musoma Mjini Mh Vincent Nyerere akiwa Visiwani Zanzibar amesema kuwa mpaka sasa idadi kamili ya watu waliopoteza Maisha kutokana na ajali ya Meli ya Sea star  bado haijafahamika.

Mh Nyerere akiongea na kituo cha redio cha  Victoria Fm cha Mjini Musoma amesema kuwa kwa mujibu wa watu waliokuwa katika meli hiyo wamesema kuwa Meli hiyo ilikuwa imebeba watu zaidi ya wale wanaotakiwa 

Mbunge huyo amesema kuwa mpaka kufikia jioni tayari watu waliokolewa walikuwa 149 huku maiti ambazo tayari zilikuwa zimepatikana zilikuwa 29.

Ameongeza kuwa kazi za uokoaji zilikuwa ngumu na hivyo kuhairisha kazi hiyo mpaka kesho huku akisema kuwa tayari Meli hiyo imezama kabisa

Taarifa zinasema Meli hiyo imezama katika eneo la Chumbe jirani na Zanzibar


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo