
Abiria wa
wakishushwa kupitia madirishani baada ya Basi la Dar Express
lililokuwa linatoka Arusha na Basi la Simba mtoto lililokuwa linaenda
Tanga kugongana uso kwa uso maeneo ya Wami kiasi cha masaa mawili hivi
yaliyopita. Mwanahabari wa Globu ya Jamii aliyekuwa eneo la tukio muda
mfupi baada ya ajali kutokea anasema hadi anaondoka mahali hapo hakuna
maafa yaliyoropotiwa ila watu kadhaa wamejeruhiwa na kuna mtu mmoja
amebanwa katikati ya mabasi ambayo kisa cha kugongana kwake bado
hakijafahamika.

Uso kwa uso

Abiria wakijaribu
bila mafanikio kumuokoa mwenzao aliyenaswa

Mmoja wa majeruhi

Mama akiwa
anaugulia pembeni mwa barabara

Abiria wakiendelea
na juhudi za kuwatoa wenzao kutoka katika mabasi hayo
Picha kwa hisani ya MPEKUZI