WAZIRI MKUU PINDA AWASILISHA MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI YAKE

Dodoma                              

Waziri mkuu Mizengo Pinda amewataka wananchi na wanasiasa kufuata sheria kanuni na taratibu za nchi ili kudumisha amani na utulivu

Waziri mkuu Pinda ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu bungeni mjini Dodoma na kusema pia kufuatwa kwa sheria na kanuni zitasaidia kudumisha amani iliyopo hivi sasa

Hali kadhalika waziri mkuu amezungumzia pato la taifa pamoja na mikakati ya kukabiliana na ongezeko la ajali za barabarani
WAKATI HUO HUO

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philip Mulugo amekiri kuwepo kwa upungufu wa waalimu katika shule za msingi na sekondari hapa nchini

Katika hatua nyingine naibu waziri Mulugo pia akatoa ufafanuzi akisaidiwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Utumishi Selina Kombani kuhusu mishahara ya waalimu 500 ambao wanadaiwa hawajalipwa, na kusema kuwa si kweli ila ni waalimu 210 ambao hawajalipwa na hii imetokana na taarifa zao kuchelewa kutumwa wizarani


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo