BASI LA PENGUIN LAPATA AJALI MAKETE


Watu 12 wamejeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari jingine na kupiduka katika eneo la Mang’oto wilayani Makete

Akizungumza na MTANDAO HUU mkuu wa polisi wilaya ya Makete Bw, Peter Kaiza amesema ajali hiyo imetokea baada ya basi la kampuni ya Penguin lililokuwa likielekea Njombe kugongana uso kwa uso na gari aina ya fuso yenye namba za usajili T 437 BAB

Bw Kaiza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni wembamba wa barabara uliopelekea magari hayo kushindwa kupishana

Aidha amesema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Consolata Ikonda kwa matibabu ambapo majeruhi 7 walitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani na wengine watano bado wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo

Na: Teddy Fabian & Ester John


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo