Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la MAMA MKENYA anayesadaiwa kupotea kwa miaka 6 amepatikana nyumbani kwa mtoto wake wa kiume katika mazingira yanayoshukiwa ni ya kishirikina.
Kituo cha redio CG FM kikiwa kwenye eneo la tukio kimeripoti kwamba mwenyekiti wa kotongoji cha mwenge FREDRICK ITOGOZYA amesema walifika eneo la tukio baada ya kupewa taarifa na wananchi kupatikana na mwanamke huyo aliyepotea miaka 6 iliyopita.
Nao baadhi ya mashuhuda na majirani akiwemo DEODATUS MBWILIZA na JUMA ALMAS ambaye pia ni mwenyekiti wa shimoni wamesema wamefika na kumshuhudia mwanamke huyo ambaye walikuwa kwenye hali mbaya kiafya na kiakili.
Diwani viti maalum wa kata hiyo ya Urambo Wilayani Urambo mkoa wa Tabora EDITHA BARNABAS amekiri kulitambua tukio hilo akisema wamelipigia jeshi la polisi ambalo lilimuijia mwanamke huyo na kumpeleka hospitali huku mtoto wake akitokomea pasipojulikana.
Chanzo:CG FM Radio