WAKAZI WA TARAFA YA MATAMBA WILAYNI MAKETE KUFURAHIA HUDUMA YA MAJI HIVI KARIBUNI

Makete                                      

Tatizo la maji lililokuwa likiwakabili wananchi wa vijiji vya Matamba, Ng’onde na Mpangala katika tarafa ya Matamba wilayani Makete sasa litapatiwa ufumbuzi ifikapo mwezi Agosti mwaka huu

Akizungumza na MTANDAO HUU katibu tarafa wa Matamba Bw, Benedict Mwageni amesema tayari mkandarasi kutoka kampuni ya gochi ya jijini Dar   es salaam amekwisha wasili na kuanza uchimbaji wa mitaro kwa ajili ya kusambaza mabomba ya maji katika vijiji hivyo

Kwa upande wao wananchi wa vijiji hivyo wamesema kuwa mradi huo ukikamilika utawaondolea adha ya kutembea umbali mrefu na katumia muda mwingi kufuata maji badala ya kufanya shughuli zingine za maendeleo

Aidha wamesema kuwa ujenzi wa mradi huo wa maji utawasaidia kuinua uchumi wao na kuboresha maisha yao kwani muda walikuwa wakiutumia kutafuta maji watafanya mambo ya kimaendeleo na pia wananchi wengine watapata ajira kupitia mradi huo.

Na: Kumbuka Kilando


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo