MGANGA WA JADI WILAYANI MAKETE ASIMAMISHWA NA SERIKALI KUTOA TIBA!

Makete

Serikali wilayani Makete imepiga marufuku shughuli za tiba asili zinazotolewa wilayani hapa na Mganga wa asili aitwaye Dkt Musa hadi hapo itakapojiridhisha na vibali vyake, ndipo itakapomruhusu

Akizungumza katika hafla kukabidhi vyeti, vitabu vya muongozo na masharti ya kazi kwa waganga wa tiba asili wapatao 10 wilayani hapa, kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Makete Boniphace Sanga, amesema wameifika hatua hiyo baada ya kuona kuwa mtaalamu huyo wa tiba asili amekiuka taratibu ikiwa ni pamoja na kutokuwa na kibali kutoka ofisi ya mganga mkuu wa wilaya

Amesema walipofika kwenye nyumba ya wageni ambayo anatolea huduma hiyo alimkuta msaidizi wake na DKt Musa ambaye alisema vibali anavyo Dkt Musa ambaye amesafiri navyo kwenda Kyela

Kwa upande wake msaidizi wa mganga huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe amekiri kufanya kazi bila kufuata utaratibu na kusema vibali vyote amesafiri navyo mkubwa wake ambaye ni Dkt Mussa na ataviwasilisha wilayani (kwa Mganga mkuu wa wilaya) pindi akifika navyo
 
Katika hotuba ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya makete Mh. Josephine Matiro iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa tawala wa wilaya Bi. Lilian Alex amekemea tabia ya waganga wengi wa tiba asilia na tiba mbadala kutosajiliwa na baraza, majengo ya kutolea huduma kutokidhi sifa, waganga wanaoenda maeneo mengine kufanya kazi bila kutembea na vibali vya usajili pamoja na kutoa matangazo katika vyombo vya habari bila kupata vibali katika mamlaka husika, na kuwataka waganga wote kufuata taratibu, sheria na kanuni za nchi katika kufanya kazi zao

Wakati wa kukabidhiwa vyeti hivyo na mgeni rasmi kila mmoja alisomewa sheria taratibu na kanuni zitakazowaongoza katika utendaji kazi wao
Na Edwin Moshi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo