Stephen Ulimboka akipakiwa katika gari la wagonjwa
baada ya kutolewa katika chumba maalum cha uchunguzi hospitalini
Muhimbili akipelekwa katika wodi ya Moi.
Baadhi ya madaktari na manesi wakilisukuma gari la
wagonjwa lililombeba Dk. Ulimboka kumpeleka Moi.
... Wakiwa nje ya mlango wa kuingilia katika
chumba ambacho aliingizwa daktari huyo.…
Stephen Ulimboka akipakiwa katika gari la wagonjwa
baada ya kutolewa katika chumba maalum cha uchunguzi hospitalini
Muhimbili akipelekwa katika wodi ya Moi.
Baadhi ya madaktari na manesi wakilisukuma gari la
wagonjwa lililombeba Dk. Ulimboka kumpeleka Moi.
... Wakiwa nje ya mlango wa kuingilia katika
chumba ambacho aliingizwa daktari huyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali
wakifuatilia tukio hilo.
Wauguzi na madaktari wakijadili tukio hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Haki za Binadamu, Hakika
Kiria, akiongea na waandishi na madaktari.
Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari nchini (MAT),
Namala Mkopi, akitema cheche mbele ya waandishi na madaktari.
Katibu wa Chama cha Madaktari, Edwin
Chitage, akiongelea tukio hilo.
Kiongozi wa madakitari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, leo ameokotwa
maeneo ya Mabwe Pande, Dar es Salaam, akiwa hoi baada ya kupigwa na watu
wasiofahamika.
Kitendo hicho kilisababisha kusimama kabisa kwa
huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya madaktari,
wauguzi na wahudumu wengine kukasirishwa na kitendo hicho.
Madaktari
wameishtumu serikali na jeshi la polisi kwa kile walichokiita kushiriki
katika jaribio la kumwua kiongozi wao.
(PICHA ZOTE ISSA MNALLY NA HAROUN
SANCHAWA, GPL) NA GLOBAL PUBLISHER