



PICHANI: Dkt. Ulimboka akiwa katika
hali mbaya mara baada ya kuokotwa akiwa hajitambui.
Taarifa iliyonifikia (JamiiForum) hivi
punde ni kuwa jemedari Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita usiku na
watu watatu waliokuwa na silaha za moto na kumpeleka kusikojulikana!
Inasemekana alipigiwa simu na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina
moja la 'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa akiwasiliana naye na kujiita
afisa wa serikali na kudai kuwa alitaka aonane naye face to face kwa
ajili ya reconciliation.
Taarifa zimekwisha fikishwa polisi na
sehemu zingine kwa ajili ya ufuatiliaji. (source chanzo cha kuaminika).
UPDATE:
Inaelekea
waliomteka si watu wema kabisa, Dr. Ulimboka kaokotwa sehemu akiwa
katika hali mbaya sana!
By Riwa:
Jamani this is is serious; Nimepigiwa
simu sasa hivi na watu wa Legal and Human Rights Center wameniambia
wametoka kumchukua Dr. Ulimboka kule Mabwepande amepigwa vibaya sana na
ni emergency wanampeleka MOI sasa hivi.
Please
tunaomba mtume habari hii kila mahali please!
Ni habari ya uhakika sana nimeomngea na Patience Mlowe wa
Legal and Human Rights center.
Chanzo:
Colleague ambaye yuko naye sasa!
Source:JamiiForum