MCHANGO WA WANANCHI KATIKA MAENDELEO YA SHULE BADO UNAHITAJIKA MAKETE

Makete

Imebainika kuwa wananchi wilayani makete wakijitolea kujenga shule zao kwa kushirikiana na kamati za shule itasaidia kuinua kiwango cha elimu katika shule zao

Akizungumza na wanahabari wetu ofisini kwake kaimu afisa elimu Bw. Mlowe Leopold amesema kwa hivi sasa serikali haitoi pesa kwa ajili ya kununulia vifaa vya ufundishaji hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana na kamati za shule ili kuweza kuwasaidia waalimu kununua vifaa hivyo  kwa ajili ya utendaji kazi

Amesema wananchi wanatakiwa kuwa tayari kuchangia fedha wakati wowote pindi watakapotakiwa kufanya hivyo na kuwaomba viongozi wa kisiasa wilayani hapa kushirikiana na viongozi wengine wa eneo husika ili kuweza kuinua kiwango cha elimu na kuweza kuwapa hamasa  katika ujenzi wa shule zao

Ameongeza kuwa wilaya inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kukabiliwa na waalimu wagonjwa ambao kwa kiasi Fulani liaathiri utendaji kazi na kusababisha huduma ya elimu kushuka kwa kiasi Fulani

Na Raphael Abel/Teddy Fabian/Ester John


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo