HONGERENI WATOA HUDUMA PAMOJA TUWALEE

Shirika lisilokuwa la kiserikali la ELCT Makete kupitia program ya Pamoja Tuwalee inayohusika na kuwahudumia watoto walio katika mazingira hatarishi limewapongeza wahudumu wanaowahudumia watoto walio katika mazingira hatarishi

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mratibu wa Programu hiyo Mch. Ezekiel Sanga amesema mpaka sasa wanahudumia watoto 2,965 kutoka katika kata 10 wilayani Makete ambazo zina vjijiji 52 ambao wanaishi katika mazingira magumu

Mch. Sanga amewapongeza wahudumu hao na kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo kwani idadi ya watoto hao inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na vifo vya wazazi wa watoto hao

Ameongeza kuwa watoto wotw wanapaswa kupewa haki zao za kimsingi ikiwemo elimu pamoja na chakula na kukemea tabia ya baadhi ya walezi wanaotumia misaada wanayopatiwa watoto hao kwa maslahi yao binafsi na kuahudi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaochukua miaada inayotolewa na shirika hilo kupitia programa ya pamoja Tuwalee

Na Timotheo Swalo na Anitha Sanga


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo