Mahakama kuu ya
Tanzania Kitengo cha kazi leo kimetoa onyo kwa Chama cha Madaktari
Nchini (MAT) kuzingatia amri ya Mahakama hiyo iliyotolewa siku ya
Ijumaa tarehe 22 Juni 2012 ya kusitisha na kutoshiriki katika mgomo na
kumtaka Rais wa Chama cha Madaktari kutangaza kutii amri hiyo kupitia
vyombo vya habari.
