CCM YASEMA IMEJIPANGA KUSHINDA KATIKA CHAGUZI NDOGO WILAYANI MAKETE

 Mwenyekiti wa CCM Taifa Mh. DKT Jakaya Kikwete

Chama cha mapinduzi (ccm) wilayani Makete kimesema kuwa kimejipanga vyema katika kuhakikisha kinapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa viongozi mbalimbali kwa ngazi ya vijiji na kata wilayani humo

Hayo yamesemwa na katibu wa wilaya wa chama hicho Bw. Miraji Mtaturu wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari wa mtandao huu ofisini kwake

Amesema chama chake kimeweka wagombea katika sehemu zote zitakazokuwa na uchaguzi ambapo wanachuana na vyama vingine vya siasa katika baadhi ya vijiji na kwamba kuna baadhi ya vijiji chama hicho kimepita bila kupingwa

Kuhusu kampeni Bwana Mtatiru amesema bado wanaendelea katika sehemu mbalimbali kama Matamba, Ng’onde na Iyoka na kuwaomba wananchi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi katika kampeni zao ili waweze kusikiliza na kuzielewa ilani za chama hicho

Aidha kufuatia uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 2 mwezi ujao wananchi wameombwa kuzitunza vizuri shahada zao za kupigia kura ili waweze kuitumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na waweze kumchagua kingozi wanaye mtaka

Na: Tatu Yassin, David Nyembe & Riziki Manfredy


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo