Wachimbaji wadogo wadogo wa madinikatika moja ya machimbo.
Na.Ashura Mohamed.Manyara
WIZARA
ya
Nishati na Madini hususan Ofisi ya madini
kanda ya kaskazini imekemea vikali
wachimbaji wa madini ambao wamekuwa wakitumia baruti kama silaha mbadala
ya
kuzitumia kama nyenzo za kazi ya
uchimbaji.
Akizungumza
na wandishi wa habari kamishna wa madini kanda ya kaskazini Mhandisi
Benjamini Mchwampaka
amesema kuwa vitendo hivyo viovu vinatokana na wachimbaji wa wasiokuwa
na
maadili ya uchimbaji madini ambao wanatumia baruti kutengeneza mabomu ya
kienyeji na kuwatupia wachimbaji wa migodi ya jirani.
Mhandishi
Mchwampaka
ameongeza kuwa ofisi yake haitolifumbia macho suala hilo kwa kuwa huo
sio uchimbaji
bali ni uhalifu kwa kuwa una lengo la kuwaumiza na kuwatisha kusudi
wawafukuze
ili kuchukua maeneo yao ambayo yanahisiwa kuwa na uzalishaji wa madini.
Aidha
ametaja
maeneo ambayo vitendo hivyo vimeshamiri
sana kwenye migodi inayopakana na moigodi ya Kampuni ya Tanzanite One
kwenye
kitalu C.
Amefafanua
kuwa
mgodi wowote ambao utabainika kwamba wachimbaji wake wanajihusisha na
vitendo
vya kuwatupia mabomu wachimbaji wa migodi jirani,mgodi huo utafungwa
mara moja
na leseni husika itafutwa na wahusika wote watachukuliwa hatua kali za
kisheria.
Pia
amewataka
Mameneja na wachimbaji kuwa ni lazima
kutangaziana baruti ama moto kabla ya
ulipuaji baruti kufanyika ili kuthibiti
vitendo viovu.
NA FULLSHANGWE BLOG