Mbunge wa Kawe Mh Halima
Mdee ameeleza kuwa wasanii wa filamu pamoja na kuwa na muonekano katika
jamii lakini wapo nyuma sana katika masuala ya kijamii, lakini jambo
baya kuliko yote ni kukosa umoja na ushirikiano katika masuala yao, hilo
ameligundua katika kuugua kwa msanii mwenzao Juma Kilowoko
‘Sajuki’.
“Wasanii wa filamu wapo nyuma sana kila mtu anajijali yeye tu
hana msaada kwa mwenzake, leo hii Sajuki anaumwa na alikuwa akihitaji
msaada wa kifedha ili akatibiwe nje ya Nchi lakini hakuna hata msanii
mmoja aliyefanya juhudi zozote hata kuchangisha fedha hizo, tatizo
lilomkuta Sajuki si tatizo la pekee yake mtu yoyote linaweza
kumkuta,”anasema Mh. Mdee.
Mbunge
huyo mwenye mvuto Bungeni na mpiganaji katika masuala ya kijamii alitoa
pongezi kwa kundi la Orijino Komedi kwa kubuni na kuvunja vipindi vyao
na kutumia muda huo kuchangisha fedha kwa ajili ya kumsafirisha mgonjwa,
pia anasema kuwa wao wanajitahidi kuibana Serikali Bungeni kuhusu
maslahi yao na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo alitoa ahadi
kuongelea maslahi ya wasanii katika bajeti mwezi wa saba.
Mh.Halima Mdee katika
kuguswa na ugonjwa wa msanii Sajuki pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya
msanii huyo, pia aliungana na wasanii wa muziki sambamba na Waheshimiwa
Wabunge katika kuimba wimbo maalumu kwa ajili ya kumchangia msanii
Sajuki huku wasanii wa filamu wakiwa wachache ambao walikuwa ni William
J. Mtitu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Wema Sepetu na Wastara Juma
pekee.
Hali hiyo ambayo hata waheshimiwa wamaeanza kuiona ni tatizo, ni
wazi wanawatetea watu walio katika makundi yasiyo na manufaa kwa wasanii
wenyewe na jamii nzima kwa ujumla hivi sasa kuna kundi la TAFF na Bongo
Movie Unity ni kundi gani linawakilisha maslahi ya wasanii wote kwa
ujumla? Badilikeni ili muondoe taswira mbaya mliyojenga kwa jamii,
hatuwezi kuwa maadui kwa kuongea ukweli...
Na Pro-24

