Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Makete Bw. Miraji Ntaturu, amewataka wakazi wa wilaya ya Makete bila kujali itikadi za vyama kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatatu, Mei 21 mwaka huu kwa ajili ya mapokezi ya mbunge wa jimbo la Makete (CCM) ambaye pia ni Naibu waziri wa maji Mh. Dkt. Binilith Mahenge, ambaye atawasili jimboni humo
Miraji amesema mapokezi hayo yameandaliwa na chama hicho kufuatia mbunge huyo kuteuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Maji, ambapo pia anatarajiwa kuhutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya mabehewani wilayani hapo
Mapokezi hayo ambayo yanatarajiwa kupambwa na pikipiki, viongozi wa vyama na serikali, pamoja na wananchi yataanzia katika mpaka wa wilaya ya Makete na Njombe kuanzia asubuhi, ambapo mbunge anatarajiwa kufika kwenye ofisi za chama hicho kabla ya kwenda kwenye Mkutano wa hadhara