RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika Warsha ya siku moja itakayojadili ukuwaji wa uchumi na
changamoto zake, itakayofanyika Mei 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam .
Akizungmza na wandishi wa
habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii Nchini
(ESRF), Dk. Bohela Lunogelo amesema wameandaa warsha ambayo inatarajiwa
kuwakutanisha wadau ambao watachangia mada mbalimbali.
Amesema mada zitakazo jadiliwa
siku hiyo zimegawanyika katika sehemu kuu tatu ambapo zote zinahusiana na
tafiti mbalimbli zilizofanyika kwa lengo la kuimarisha ukuaji uchumi katika
jamii.
Dk. Lunogelo amesema ukiachilia
mbali Rais pia atakuwepo Profesa Benno Ndulu ambaye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania na Dk. Huang Chengwei ambaye ni
mtaalamu anashughulika na kuondoa umasikini nchini China .
Adha, amesema mambo ya
takayojadiliwa na wataalamu siku hiyo yatakuwa ni pamoja na madini ukuaji wa
viwanda na utalii maswala ya usimamizi wa ardhi na ukuaji wa kilimo.Mengine ni
kuhusiana uongozi, utawala bora na maswala ya miundombinu na uendeleza wa
rasilimali na mengineyo.