
Bi Emelda Taikwa Adam, Afisa Mazingira
mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu wa Rais Akiwasilisha maoni ya Tanzania
katika masuala ya Kilimo na mabadiliko ya Tabia nchi, katika mkutano wa
sayansi ya Taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi unaendelea mjini Bonn
Ujerumani
Akiwasilisha maoni hayo, katika Mkutano huo Afisa
Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya makamu wa Rais Bi Emelda Taikwa Adam
ameeleza kuwa, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zinatakiwa kuangalia zaidi
katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ili kuweza kuongeza uzalishaji na
kuhakikisha usalama wa chakula kupitia sekta ya kilimo kwani ndo uti wa mgongo
wa Taifa.
Bi Emelda aliongeza kuwa, katika kuhimili mabadiliko ya
Tabia nchi Tanzania
kupitia sekta ya kilimo na tafiti zilizokwisha fanyika kuonyesha kuwa kuna
matumizi salama ya mbegu zinazohimili ukame, pamoja na matumizi sahihi ya
kilimo cha umwagiliaji, na kuna kila sababu ya matumizi ya teknolojia zaidi ya
kisasa na kujenga uwezo kwa wakulima wa kawaida ili kuweza kuhakikisha usalama
wa chakula.
Akizungumzia athari za mabadiliko ya Tabia nchi katika
sekta ya kilimo bi Emelda amesema kuwa, kupungua kwa mvua kunakopelekea ukame
nchini na kuongezeka kwa gesi joto kumeathiri kwa kiasi kikubwa sana sekta ya
kilimo, na katika kupunguza gas joto katika kilimo kunahatarisha usalama wa
chakula na kupoteza ardhi kwa wenyeji.
Ameongeza kuwa pamoja na kwamba sekta ya kilimo imekuwa na
mikakati mbalimbali inayotekelezeka katika kuhimili mabadiliko ya tabia nchi, Tanzania
inatakiwa kuwa na mfumo ambao utahakikisha kuwa upunguzaji wa gesi joto katika
kilimo unatokana na jitihada za kuhimili mbadiliko ya tabia nchi.
kwa hisani ya H@ki ngowi