WANAKIJIJI WA ENGORORA WANAKABILIWA NA UHABA WA NYUMBA ZA KISASA


 NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA


WANANCHI wa kijiji cha Engorora katika kata ya Kisongo Mkoani hapa kinakabiliwa na changamoyo ya uhaba wa nyumba bora ambapo kijiji kizima kina watu 3000 wakati nyumba bora zikiwa ni 100

Hayo yalielezwa kijijini hapo na Mwenyekiti wa kitongoji cha Engorora kati Bw Piniel Lengai alipokuwa akizugumza na FULLSHANGWE kuhusiana na changamoto hasa za makazi bora

Bw Lengai alisema kuwa uhaba wa nyumba bora amnbao unaikabili sana kijiji hicho unatokana na uhaba wa Vipato mbalimbali vya uchumi hali ambayon inasababisha kwa kiwango kikubwa sana makazi duni

“ndani ya kijiji chetu ambacho hakipo mbali sana na mjini hamna nyumba bora nzuri kwa kuwa tunakabiliwa na changamoto mbalimbali na uhaba huu wa nyumba ambazo si nzuri pia ni kikwazo kwetu hasa na kwa hali hiyo  hii ni changamoto kubwa sana”alisema bw Lengai

Katika hatua nyingine alisema kuwa pia kijiji hicho kinakabikliwa na changamoto ya kutokuwepo kwa magala ya kuhifadhia Chakula na Mazao mbalimbali hali ambayo inafanya mazao mengi kuharibika sana, hasa wakati wa mavuno

Alifafanua kuwa hasara ambazo wanazipata kutokana na uhaba wa maghala ni pamoja na kuchezea chakula kingi bila mipangilio maalumu kwa kuwa  asilimia kubwa sana ya wananchi hawana sehemu maalumu ya kuhifadhia chakula hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana baa la njaa hasa wakati ambao hamna chakula cha kutosha

Mbali na hayo alisema kuwa Serikali inatakliwa kuhakikisha kuwa inawekeza zaidi vijijini kwa kuhakikisha kuwa wanapata huduma zote imara ikiwemo michakato ya elimu mbalimbali kama vile elimu ya masuala ya uchumi,uzazi na hata afya kwa kuwa wengi wa wananchi wanapata adha mbalimbali kwa uhaba wa  elimu za kijamii.

Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Joseph John alisema kuwa endapo kama huduma mbalimbali zitaboreshwa kijijini hapo basi ni wazi kuwa kijiji hicho kitaweza kuwa mstari wa mbele sana katika kuleta mabadiliko makubwa sana hasa kwa upande wa Mazao na Mifugo kwa kuwa uwezo mkubwa bado wanao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo