CANDY CALIFORNIA AACHIA NGOMA YAKE MPYA…..2012!!

HELLEN DAVID (Candy) ambaye alikuwa miongoni kwa washiriki katika kinyang`anyiro cha kumsaka mshindi wa “Tikisa 2011” na kutolewa katika hatua za mwisho za shindano lile, ameachia Track yake mpya inayoitwa “NIMPENDE MILELE” chini ya kampuni ya  Most Record&Production ya jijini dar  es salaam.
Hellen au kwa jina la kisanii anaitwa "Candy California” ni msanii ambaye anavipaji vingi, licha ya uwezo wake mkubwa wa kucheza muziki wa kila aina pia ana uwezo mkubwa sana wa kuimba. Most Record & Production waliona kipaji chake ndipo hawakusita kumpa ofa ya kurekodi nyimbo pamoja na video.
Baada ya ofa hii aliyopewa na Most  Record & Production, "Candy California”  amepata ofa nyingine ya kurekodi nchini Afrika ya Kusini mapema mwezi Juni 2012, ataweka wazi pale mipango yote itakapokuwa sawa.

CAND PROFILE:
JINA KAMILI:  HELLEN DAVID LUSEKERO
JINA LA KISANII: CANDY CALIFORNIA
PHONE NO :- 0753 915938
WIMBO WAKE UNAITWA : NIMPENDE MILELE
STUDIO : MOST RECORD RECORD
PRODUCER: SAM BABYLONE
EMAIL/FACEBOOK :-   hellendavid40@yahoo.com
Picha za chini zinaonyesha shooting ya video ya wimbo wake mpya unaitwa  “Nimpende Milele” ni video ambayo inayoshutiwa na kusimamiwa na Most Production ni video ambayo itakuja na mtazamo tofauti kwakweli ni video kali sana..!



Candy California akiwa kwenye acting na hisia kali kwenye shooting ya wimbo wake “nimpende milele” 


Hapo Candy California akishoot moja ya vipande vya video hiyo
Candy kushoto pamoja na group lake kwenye pozi

Candy California akiwa kwenye pozi…!!






JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo