DSM 04.04.2012
Wasimamizi wa chuo cha mafunzo ya biashara cha CBE kilichopo jijini DSM wameanza kutekeleza sera mpya inayozua utata kuhusu mavazi ya wanafunzi chuoni
Sera hiyo inapiga marufuku wanafunzi wa kike kuvalia sketi fupi na suruali ndefu zinazowabana pamoja na kuwapiga marufuku wanafunzi wa kiume kusuka nywele
Mwanafunzi atakayekiuka sera hiyo ataadhibiwa kwa kufukuzwa darasani kwa kipindi cha miezi mitatu
Uamuzi huo umefuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wazazi wanafunzi wenyewe na hata waalimu kuhusu suala zima la maadili hususana upande wa mavazi katika chuo hicho
Wapo baadhi ya wanafunzi chuoni hapo ambao wamekubaliana na sera hiyo huku wengine wakiipinga sera hiyo na kuutaka uongozi wa chuo hicho kushughulikia masuala mengine ya taaluma chuoni hapo na si mavazi