MAKETE
Jumuia ya wanafunzi kutoka katika makanisa ya kipentekoste Tanzania CASFETA wilayani Makete wamefungua rasmi kongamano la Pasaka (EASTER CONFERENCE katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Iwawa.
Akifungua kongamano hilo Mwangalizi wa Makanisa ya Tanzania Assembles of God sehemu ya Tandala Mch. JONASI SANGA amekemea vitendo viovu vinavyofanywa miongini mwa wanafunzi kitendo alicho kiita ni dhami.
Amevitaja vitendo viovu vinavyofanywa na wanafunzi mashuleni kuwa ni pamoja na ulevi uashereti, wizi pamoja na vurugu wanapokuwa mashuleni na kuwasihi kuwa waadilifu kwa walimu na wazazi pamoja na kuwa na juhudi katika masomo yao
Katika hatua nyingine ametaka wanafunzi waliookoka kuwa mfano wa kiugwa na kutumia maandiko matakatifu kama silaha yao ya imani ya kikristo na kuongeza kuwa Biblia imeandikwa shika sana Elimu usimwache aende zake, hivyo wanafunzi hao wazingatie elimu
Na Aldo Sanga & Anitha Sanga