TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUPAMBANA NA UKIMWI NA KIFUA KIKUU

Watoa huduma shirikiishi wa kifua kikuu na UKIMWI wamekutana kujadili mikakati ya kupambana na magonjwa hayo yanayoendelea kuwa changamoto katika wilaya ya Makete na taifa kwa ujumla mjadala uliofanyika katika ukumbi wa hospitali ya wilaya ya Makete

Akifungua kikao hicho Afisa Afya kutoka hospitali ya wilaya ya Makete Bw. Felician Chawala amesema tatizo la ugonjwa wa Ukimwi na kifua kikuu ni magonjwa ya kuambukiza hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anapambana ili kuokoa kizazi kilichopo na kijacho ili kutekeleza dhana iliyopo kuwa Tanzania bila UKIMWI inawezekana

Katika kikao hicho baadhi ya watoa huduma kutoka vituo vya Matamba, Hospitali ya Consolata Ikonda, zahanati ya Lupalilo pamoja na hospitali ya wilaya ya Makete wametoa changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na watu kuwa na ukaidi wa matumizi sahihi ya ARV, mila na desturi potofu pamoja na imani za kidini zilizopo kwa watu

Naye mratibu wa kifua kikuu
na Ukimwi Dr.
Michael Ntaho amesema wanategemea kuunda vikundi pamoja na kutumia vyombo vya habari ili kutoa elimu kwa jamii
Na Aldo Sanga   


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo