Na Kenneth Ngelesi, Mbeya
WANANCHI wenye hasira kali katika kitongoji cha Itezi Magharibi, katika kata ya Itezi, Jijini Mbeya, jana walichukua uamuzi mgumu wa kumzika akiwa hai, mkazi mwenzao Nyerere Kombwee, wakimtuhumu kuwa ni mchawi wakimhusisha na kifo cha mtoto wa mdogo wake siku moja kabla.
Tukio hilo lilitokea jana katika Kitongoji hicho , ambapo wananchi hao walimkamata na kumpeleka sehemu walipo kuwa wakichimba kaburi na kumlazimisha na kumtaka ainingie ndani ya kaburi ililikuwa likiandaliwa kwa ajili ya kumzika mtoto wa kaka yake, aliyetajwa kwa jina la Leonard Kombwee na kwamba alipokubali walimpiga na jiwe kichwani na hatimaye kumfukia akiwa hai.
Ina daiwa wakati wakiwa katika shughuli za kuchimba kaburi hilo kwa ajili ya kumzilka mtoto wa kaka yake wananchi hao walianza kujadili baada ya kuona marehemu hayupo sehemu ya tukio ndipo wa teuana miongoni mwao kwenda kimfauta kwake walipo fika kwa hawakumkuta wakaanza kutembeza kipigo kwa mamam yake mzazi na dada yake ili wataje maali alipo mwanae huyo.
Baada ya kipigi hicho mama mzazi na dada marehemu waliwapekeka maala alipo walipo mkuta wakampa kipigo na kuamurua aongozane nao kwenda kuchimba kaburia mtoto wa kaka yake.
Inadaiwa kuwa marehemu huyo wa pili alizikwa akiwa hai majira ya saa 3;00 asubuhi na haikufahamika alidumu kwa muda gani akiwa hai kwani hadi polisi na viongozi wakata walipoutawanya umati wa wananchi kwa risasi na kuamua kufukua kaburi hilo majira ya saa 8:00 mchana walimkuta tayari amekufa.
Baadhi ya majirani wa familia hiyo walidai kuwa tukio hilo limesababishwa na ugomvi wa kifamilia ambao umedumu kwa muda mrefu, ambapo inadaiwa marehemu Nyerere alikuwa akituhumiwa kumuua mtoto huyo wa kaka yake na ndipo wananchi wakaamua kulipa kisasi.
Walidai kuwa baada ya marehemu Leonard kufariki siku ya Aprili 27 majira ya saa 3:00 asubui katika kifo kilichokuwa cha utata walimshuku marehemu baba yake mkubwa kwani hakwenda kwenye msiba.
Walisema baada ya kufuata nyumbani kwake marehemu Nyerere alikutwa amejificha walipo mbana mama yake alisema kuwa alikuwa amejificha ndani ya moja ya nyumba zake , hali iliyowalazimu kubomoa na kumshushia kipigo kikali wakimlazimisha kwenda kushiriki kuchimba kaburi la marehemu mtoto wa kaka yake.
Aidha sababu liliyo wapelekea wanachi hao kumzika akiwa hai ni kutokana na Nyerere kutoa vitisho kwa wananchi hao akiwaonya kuwa kipigo walichompatia na kusababisha amwage damu hakitaenda bure ndipo kiliwapandisha hasira na walipofika katika eneo la makaburi , walikuta likiwa lina urefu wa futi zaidi ya tatu.
Walimlazimisha kuingia ndani ya kaburi hilo na alipoingia tu mmoja wa wananchi hao alimpiga na jiwe zito kichwani huku mwingine akimkandamiza na Chepeo hali iliyosababisha kushindwa kujinasua na kufukiwa kirahisi akiwa mzima.
“Baada ya kuona mchanga unazidi kujaa huku akiwa amekandamizwa na Chepeo marehemu aligeuka na kulala kifudifudi hadi mchanga ukajaa kaburi” alieleza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyeomba jina lihifadhiwe.
Diwani wa kata hiyuo, ambaye pia ni Naibu Meya wa Jiji la Mbeya, Frank Maemba, ambaye alikuwa eneo la makaburi kusimnamia hali ya amani huku mwili wa marehemu ukiwa ndani ya Kaburi hilo ukisubiri wataalamu wa afya kuufanyia uchunguzi kabla ya kuzikwa.
Alikiri kuwa tukio hilo ni la kikatiri na halikupaswa kufanya na wananchi na kwamba wote walioanzisha maamuzi ya kuwashawishi wenzao kujichukulia sheria mkononi watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
Mbali na hilo Diwani huyo alitoa wito kwa wananchi kuepuka kuweka wazi migogoro ya kifamilia katika jamii isiyo husika tatizo kam hilo limesababishwa migorogro ya kifamila kufahamika kwa watu wasio husika.
‘Ni vema migorgoro ya kifamilia ikatatuliwa na wanafamilia wenyewe kwani bila hivyo matatizo ndo kama haya kwani inaonyesha kumekuwepo na ugomvi kwa muda wa siku nyingi lakini kama familia hawakuchua jukumu la kulitatua na matokeo ndo hayo, inaumiza sana kupoteza watu wawili wa familoia moja tena kwa masula yasiyo na msingi” alisema Maemba
Askari waliofukua kaburi alikofukiwa marehemu walilazimika kutupa mapomu ili kuwatawanya wananchi ambao baada ya kumzika mwenzao akiwa hai walibaki eneo hilowalifika eneo hilo wakitumia gari aina ya Cruiser lenye namba za usajili DFP 474.
|
HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 14,2025
3 hours ago