Marehemu Bingu wa Mutharika
Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika amefariki dunia mara baada ya kuugua ugonjwa wa moyo
Kifo hicho kimetokea baada ya kukimbizwa hospitali ya mjini Lilongwe mji mkuu wa nchi hiyo baada ya kuanguka ghafla na kuzirai
Hali hiyo ilimpelekea rais Mutharika kuwa mahututi hadi mauti yalipomkuta
Mwanzoni redio ya taifa ilikuwa imetangaza kuwa mutharika mwenye umri wa miaka 78 angelipelekwa Nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi
Taarifa zinasema raisi huyo ilibainika amekwisha fariki dunia muda mchache baada ya kufikishwa hospitalini hapo kwani hali yake ilikuwa mbaya
Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo makamu wa rais Joyce Banda ndiye anayechukua nafasi ya mkuu wa nchi ingawa kuondolewa kwa banda kutoka chama tawala mwaka 2010 kunaweza kutatiza kipindi cha mpito
Hivi karibuni marehemu Rais Banda alikuwa akituhumiwa kushindwa kuongoza na kutokuendeleza uchumi wa nchi hiyo
Inasemekana alikuwa akimtayarisha mdogo wake Waziri wa mambo ya nje Peter Wamutharika kuwa mrithi wake