Makete
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Zainab Ahmad Kwikwega amewataka wafanyabiashara wanaouza soda wilayani Makete kuacha kuuza soda moja sh. 700 na badala yake kuuza bei ya zamani ya sh. 500
Mh Kwikwega ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii na kusema katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka wafanyabiashara hao wanatakiwa kuuza soda kwa bei ya sh. 500 kwa soda moja ili wananchi waweze kusherehekea sikukuu hiyo kwa furaha
Ameongeza kuwa mara baada ya sikukuu ya pasaka kumalizika Afisa biashara wilaya ya Makete atakutana na wafanyabiashara hao kujadiliana kwa pamoja sababu zilizopelekea soda kupanda ghafla na kuuzwa sh. 700 badala ya 500 na mwishowe wawe na azimio la pamoja
Maagizo hayo ya Mkuu wa wilaya yametokea kufuatia wafanyabiashara wilayani hapo kupandisha ghafla bei ya soda kutoka sh. 500 hadi 700 kwa soda moja hali iliyozua manung’uniko miongoni mwa wateja wanaotumia vinywaji hivyo