DIWANI WA CCM AFUNGWA JELA MIEZI MITATU

Na  Israel Mwaisaka,Kyela

MAHAKAMA ya wilaya Kyela mkoani Mbeya imemhukumu diwani wa kata ya Ngonga (CCM) Bw,Kileo Kamomonga kwenda jela miezi mitatu na wenzake saba huku wengine watatu wakihukumiwa kifungo cha nje cha miezi mitatu kwa  kosa la kuingia kwa jinai kwenye shamba la Bw,Grayton Mwakyanjala

Akitoa hukumu hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Bw,Joseph Luambano amesema kuwa watuhumiwa wote kwa pamoja waliingia kwa jinai kwenye shamba la Bw,Grayton Mwakyanjala huku wakijua kuwa ni kosa kisheria

Alisema kesi hiyo ambayo ni rufani kutoka katika mahakama ya mwanzo Kyela mjini iliwapatia ushindi watuhumia ambapo katika baraza la kata mrufani alishinda kwa kuzingatia kanuni hivyo baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pande zote mbili watuhumiwa wote kwa pamoja walikutwa  na hatia na kutengua  hukumu ya mahakama ya mwanzo

Hivyo kwa mujibu wa sura ya 16 kifungu cha 299 ya mwaka 2002 sheria ya kanuni ya adhabu (Pinecode) imewatia hatiani watuhumiwa

Waliofungwa jela pamoja na diwani huyo ni,Lugano Mwambola,Bosco Mwakinge,Edwin Mwakipesile, Bwigwine mwampeta, Amibu Mwampuga, Godfrey Mandolina Burton Mwambola

Waliofungwa kifungo cha nje ni Bw,Amulike Mwakisulu,Mojala Mwakigonja na Sitivini Mwaikasu ambao kwa mujibu wa hakimu huyo ni kuwa wamewekwa kifungo cha nje kutokana na umri walionao
                                               


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo