MAKETE.
Tatizo la maji lililoikumba shule ya Sekondari Iwawa limepatiwa ufumbuzi baada ya Mkuu wa Wilaya ya MAKETE Mh.ZAINABU AHMADY KWIKWEGA Kuagiza Mamlaka ya Maji kuyafungua maji yaliyokuwa yamefungwa kwa kipindi cha miaka miwili Shuleni hapo.
Akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Maji Wilaya ya Makete Mh.Kwikwega amesema Tatizo la kukatiwa Maji katika Shule ya Sekondari Iwawa limesababishwa na Kujisahau kwa baadhi ya Viongozi husika katika ulipaji wa bili za Maji hadi kufikia kukatiwa kwa huduma hiyo katika Shule ya Sekondari Iwawa
Aidha Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Iwawa Bw FODENI MADYEDYE amekiri kutokea kwa tatizo la Maji katika Shule hiyo na kusema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili wanafunzi wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenda kutafuta Maji nje ya eneo la Shule jambo linalopelekea kukosa vipindi na kushuka kitaaluma katika masomo.
Kwa upande wake Meneja wa mamlaka ya Maji Makete mjini Bw, JONASI NDOMBA amesema ni utaratibu wa mamlaka ya maji kumkatia mteja huduma ya Maji pindi Mteja anapo kuwa ameshindwa kulipa ankara ya maji kwa wakati hukatiwa Maji kama hatua ya kumkumbusha Mteja kulipa bili kwa wakati
Kupitia jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Kwikwega kuagiza Malaka ya Maji kufungua huduma ya Maji katika Shule ya Secondari Iwawa wanafunzi pamoja na familia za walimu wameanza kunufaika na huduma ya maji kupitia Mamlaka ya Maji wilaya pamoja mradi wa maji ulio fadhiliwa na kanisa Katoliki Makete.
Na:Anitha Sanga &Aldo Sanga.