WANAWAKE WATATU WAKAMATWA WAKIIBA PESA KWENYE DUKA LA GESI!!


Jana majira ya saa kumi na moja jioni wanawake watatu ambao majina yao hayakufahamika mara moja waliponea kwenye tundu la sindano kuuwawa na wananchi wenye hasira kali maneneo ya ITV Mwenye baada y kuiba katika duka la gesi kwa kumrubuni muuzaji kabla ya kubainika.
Wezi hao waliingia dukani hapo wakijifanya wateja na kuanza kufanya kufanya uhalifu ambapo walifanikiwa kuchukua kiasi cha shilingi laki sita ambapo walishtukiwa kabla ya kuondoka na kufungiwa dukani humo kabla ya polisi kufika eneo la Tukio na wananchi kutaka kuwachoma moto.Kulia mwenye nguo nyeusi ni muuzaji wa duka hilo.


Hapo askari wakijaribu kuzuia raia wasivunje geti kuingia ndani kuwatoa wahalifu



Hata baada ya purukushani kutaka kuwaonyesha sura zao waligoma kufunua vitambaa hapo wameloa jasho na kukauka kwa kulia



Polisi walifanyikiwa kuwaingiza ndani ya gari chini ya ulinzi mkali na vurugu za wananchi waliokuwa wanarusha mawe.
Wananchi wakiwa ''wamepaniki''

PICHA NA HABARI KWA HISANI YA MARYGORETHRICHARD BLOG


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo