MAKETE
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh.ZAINABU AHMADY KWIKWEGA, ametembelea miradi ya ujenzi wa nyumba mbili za maafisa wa jeshi la MAGEREZA, ambazo zimejengwa kwa nguvu ya Gereza la NDULAMO (w) MAKETE.
Ujenzi huo wa nyumba mbili na ukarabati wa bweni la wafungwa umefikiia hatua ya umaliziaji ambapo mkuu wa wilaya ya Makete Mh.KWIKWEGA amtoa mchango wake wa kiasi cha Tsh. milioni moja na laki tatu.
Akizungumza na wafungwa wa gereza la NDULAMO Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Kwikwega amekabidhi cherehani kwa ajili ya wafungwa pia amemshukuru mkuu wa jeshi la Magereza Tanzania KAMISHINA JENERALI AUGUSTINO NANYARO kwa kutoa ushirikiano wa kutoa Sare za wafungwa na kuahidi kujenga nyumba moja kwa ajili ya maafisa wa jeshi la Magereza.
Akitoa shukrani kwa mkuu wa wilaya ya Makete Mkuu wa Gereza la Ndulamo (W) SP. MWAKIJUNGU, ameshukuru jitihada za mkuu wa wilaya ya Makete katika kusaidia baadhi ya vifaa alivyotoa na ujenzi wa nyumba kwa maafisa wa jeshi la magereza.
SP. MWAKIJUNGU ameongeza kwa kutoa taarifa ya ujio wa vifaa vya gereza zikiwemo sare na kutambua jitihada za makusudi za Mkuu wa wilaya ya Makete kutembelea gereza hilo.
Na Aldo Sanga