Bagamoyo
Hivi sasa Tanzania ipo katika mchakato wa kuunda katiba mpya ambapo wananchi na vikundi mbalimbali wamekuwa wakiendesha mikutano na midahalo ili kupata maoni ya wananchi
Katika kutekeleza hayo mtandao wa asasi za kiraia wilayani Bagamoyo mkoani Pwani BANGONET umeendesha midahalo mbalimbali katika jimbo la Bagamoyo na Chalinze kwa lengo la kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki kutoa maoni katika kuandika katiba mpya
Katibu mtendaji wa BANGONET Leonard Peter amezungumzia baadhi ya maoni yaliyotolewa na wananchi ikiwemo kugundulika kuwa takriban asilimia 10 kati ya asilimia 100 ndio wanaotambua katiba