Makete
Wananchi wilayani Makete kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya serikali na yasiyo ya kiserikali yameombwa kuchangia vituo vya elimu ya awali kwa watoto
Hayo yamezungumzwa na Afisa ustawi wa jamii wilayani Makete Bw. Leonce Panga, nakusema kuwa ni muhimu watoto wakapelekwa katika vituo vya kupatia elimu ya awali kabla ya hawajafikia umri wa kuanza elimu ya msingi
Amezitaka serikali za vijiji kuandaa mikakati ya kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na kituo kimoja cha watoto hao wadogo kwa ajili yakufundishwa vitu mbalimbali
Aidha amesema kuwa kuwepo kwa vituo hivyo kutasaidia watoto kuwa na uelewa mzuri wanapoanza elimu ya msingi na walimu kupata urahisi wa kuwafundisha kwa kiwango kilicho bora
Na: Zuhura Sanga & Deo Mgina