Waumini wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya kusini kati wameaswa kuwa na moyo wa upendo na uchamungu hata baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwaresma
Hayo yamezungumzwa na askofu mteule wa kanisa hilo Bw,Levis Sanga, ambapo pamoja na mambo mengine amesema kuwa waumini wengi huonesha moyo wa upendo na uchamungu wakati wa kwaresma lakini baada ya kipindi hicho kuisha waumini huacha kabisa mambo hayo jambo ambalo amesema halimpendezi mungu
Aidha ameeleza kuwa kipindi hiki cha kwaresma ni wakati wa waumini kutubu dhambi zao ili kujiandaa kupokea ufufuo wa yesu kristo ambao unaitwa ushindi wa kristo duniani
Hata hivyo amewataka waumini wenye mali hususani rasilimali mbalimbali kama vipaji na ardhi basi wavitumie kwa usawa
Na:Enesta Ndille,Anitha Sanga, Riziki Manfred