Makete
Vijana wilayani Makete wametakiwa kuwa na mwamko katika kupanda miti mbalimbali ambayo itawasaidia kwa kujiongezea kipato na kuboresha mazingira pia
Hayo yamesemwa na Afisa misitu wa wilaya ya Makete Bw. Alphibian Sanga alipokuwa akizungumza na mtandao huu nakusema kuwa kwa kufanya hivyo wanaweza kujikwamua kiuchumi wao na taifa kwa ujumla
Bw. Sanga pia amewaomba wananchi kuitumia elimu wanayopewa ya kupanda miti ili kupata mazao mengi itakayowapatia mbao za kutosha kupitia misitu hiyo
Hata hivyo ametoa onyo kwa wale wanaochoma misitu kwa makusudi waache tabia hiyo mara moja na yeyote atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kwenda jela ama kulipa faini isiyopungua milioni moja
Na:Obeth Ngajilo