Wananchi wa wilaya ya Makete wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kupima ugonjwa wa kifua kikuu ili waweze kupata tiba kwa kuwa ugonjwa huo hutibika iwapo itagundulika mapema
Hayo yamesemwa na mratibu mkuu wa kifua kikuu na ukoma wilayani Makete Dk. Imanuel Ngala alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yanayofanyika Machi 24 ya kila mwaka
Amesema maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Mtwara