Kufuatia kero iliyokuwa ikiwakera wakazi wengi wanaotumia huduma za kiafya katika hospitali ya wilaya ya Makete kuhusu ubovu wa barabara iendayo hospitalini hapo, suala hilo limetolewa ufafanuzi na uongozi wa hospitali hiyo
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, kaimu mganga mkuu wilaya ya Makete Boniface Sanga amesema barabara inayolalamikiwa kuwa ni mbovu, sio barabara rasmi ya kuingilia hospitalini hapo, na badala yake barabara rasmi ya kuingilia hospitalini hapo, ni iliyopo njia panda ya Isapulano na Bulongwa eneo la Kona Makete mjini
Ufafanuzi huo umetolewa na kaimu Mganga mkuu huyo kufuatia moja ya msikilizaji wa Kituo hiki kutoa kero yake kuwa barabara inayotumika kwenda hospitalini hapo ni mbovu