Wanawake wilayani Makete wametakiwa kuuwatunza watoto yatima na kuwapa mahitaji muhim bila ubaguzi
Hayo yamezungumzwa na mwanawake anaye jishughulisha na biashara ndogondogo wilayani hapo ambaye hakutaka jina lake litajwe na kusema kuwatunza watoto yatima nakuwapa mahitaji muhimu itasaidia kuepukana na watoto wa mitaani na kuwafanya watoto hao kuishi kwa amani
Hata hivyo amesema baadhi ya wanawake wamekuwa hawawathamini watoto yatima nakupelekea baadhi ya watoto hao kuamua kuishi maisha ya kujitegemea hali inayo pelekea kuona maisha magumu na kujiingiza katika makundi mabaya kama wizi, na ulevi.
Aidha amewataka wananchi waone umuhimu wa kuwapeleka watoto yatima shule ili kuwajenga kielimu
NA ZUHURA SANGA