DSM
Ugonjwa wa malaria unaongoza kwa kusababisha vifo vingi nchini na takwimu za mpango wa taifa wa kudhibiti malaria zinaonesha watu 60,000 hupoteza maisha kila mwaka na huchangia asilimia 80 ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 na mama wajawazito
Kutokana na hilo wizara ya afya na ustawi wa jamii ilianzisha mradi wa kudhibiti malaria katika maeneo ya makazi ili kuua vimelea vya mbu waenezao ugonjwa huo waitwao anopheles ambapo watendaji wake hupita katika maeneo ya mazalia ili kuziangamiza
Hata hivyo baadhi ya wafanyakazi wa mpango huo wamegoma na kufika katika ofisi za afisa mtendaji kata ya Ilala ili kuishinikiza serikali kuwalipa mishahara yao ya miezi miwili