Moja ya barabara za mitaa zikiwa zimeharibiwa na maji kutokana na mifereji ya kupitishia maji kuziba
Wananchi wametakiwa kushirikiana na serikali kuboresha miundombinu ya barabara za mitaa hasa nyakati za mvua za masika kwani zinakwamisha mambo mengi ya maendeleo katika jamii
Hayo yamezungumzwa na mwenyekiti wa shirika la MASUPHA Benito Chengula katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu
Amesema kutokana na uharibifu wa barabara hasa zinazounganisha vijiji mbalimbali wilayani Makete kumeliathiri shirika lao kwa kiasi Fulani kwani wanashindwa kupeleka elimu ya ukimwi kutokana na barabara hizo kutopitika kwa gari kiurahisi