MNAOMKUBALI NATURE KAZI KWENU

Baada ya kimya cha muda mrefu Juma Kassim Nature ameibuka na kudai mwaka huu ni wake na anataka kurejesha heshima ya miziki wake.

Nature ambaye pia ni kiongozi wa Wanaume Halisi amesema kundi hilo limekamilisha albamu yao ambayo wataitaja miezi michache ijayo, lakini baadhi ya nyimbo tayari zipo redioni zikifanya vizuri.

Muda mwingi nilitulia na wenzangu tulikuwa tunaangalia upepo unavyokwenda na jinsi ya kuibuka tena na kufanya mambo ya uhakika zaidi, kukubalika na mashabiki hasa wa Afrika Mashariki, hatuangalii Tanzania peke yake.

Staa huyo alisema kwa ushirikiano wa Dollo, Richie One, JB aliyekuwa Mabaga Fresh, Bob Q, D. Chief, Malipo, Kaka Man, Mzimu na Eddo wanakuja na kazi za mseto ambao mashabiki watajionea tofauti na kuamua.

Nyimbo ambazo tayari zimekamilika ni 'TMK', 'Able' na 'Mguu nje Mguu ndani remix' ambapo kazi kubwa imefanywa na Dolo, KR Mullah na JB.

Nature anasema 'Halisi Studio' ni mali yake na itatumika kutengeneza zake na za kundi.

Amekiri kuwa studio yake ni ya kawaida kwa mtazamo wa haraka lakini ina vifaa vichache vyenye uwezo mkubwa na baadhi ya wasanii wameanza kufanyia kazi na wanataka kujiondoa katika mfumo wa kutegemea studio za watu.

Studio ipo wazi kwa wasanii wote na siyo Mwanaume Halisi pekee,anasema Nature na kuongeza kuwa licha ya yeye kuwa ndiye prodyuza, lakini wenzake katika kundi pia wanafanya kazi hiyo na wana mpango wa kumpata mtaalam zaidi.

SOURCE: DARHOTWIRE


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo