MAKETE
Imebainika kuwa kukosekana kwa elimu ya ukimwi katika jamii wilayani Makete, kunapelekea kuongezeka kwa maabukizi ya mapya ya virusi vya ukimwi wilayani hapo
Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi wa shirika la MASUPHA linalojihusisha na watu wanaoishi na vvu wilayani hapo Bi Aida Chengula wakati wa mafunzo ya unyanyasaji wa kijinsia jinsi yanavyopelekea maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi na kuongeza kuwa unyanyasaji huo uanatokana na jamii kukosa elimu ya ujinsia
Aidha amewaomba wawezeshaji haki jamii wa shirika hilo la MASUPHA kuwa na mwitikio mkubwa wa kutoa elimu kwa wanajamii pamoja na kutatua matatizo yao hususan unyanyasaji wa kijinsia
Amesema kuwa huu ni mwanzo wa mradi wao wa kuelimisha jamii lakini wamejipanga kuhakikisha elimu ya unyanyasaji wa kijinsia inawafikia wananchi wote