Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Makete Bi Imelda Ishuza
Makete
Wafanyabiashara na wananchi wa wilaya ya Makete wamepokea kwa mitazamo tofauti kauli iliyotolewa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete Bi Imelda Ishuza kuhusu kutokuwepo kwa soko la Makete mjini siku ya Alhamisi 02.03.2012
Wakizungumza na mwandishi wetu wafanya biashara hao wamesema kuwa wamesikitishwa na hatua hiyo kwani imekuwa na usumbufu kwao na pia inapelekea wao kukosa wateja kwani wateja wengi wamezoea siku za soko kuwa ni Alhamisi na Jumapili
Kauli hizo zinafuatia tangazo lililotolewa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete BI Imelda Ishuza kuwa soko la alhamisi ya wiki hii halitakuwepo na badala yake litakuwepo siku ya Ijumaa tarehe tatu mwezi huu kutokana na siku hiyo kuwa siku ya mnada ambao huwaalika wafanyabiashara mbalimbali kutoka ndani na njea ya wilaya kuja kuuza bidhaa zao
kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wilaya ya Makete Imelda Ishuza amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kwani utaratibu wa halmashauri ni kuwa kila Siku ya soko la kwanza la mwezi husika utaratibu hubadilika kwani huwa ni mnada unaowaalika wafanyabiashara wa ndani na nnje ya wilaya ya Makete mnada ambao hufanyikia katika soko la Ngiu na si Makete mjini kama ilivyo kawaida
Amesema wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia utaratibu huo kutokana na soko la Ngiu ambalo liko nje kidogo ya Makete mjini kuwa mbali lakini ndio maana halmashauri imeweka utaratibu wa soko hilo kutumika mara moja kwa mwezi ambapo ni kila mwanzo wa mwezi