Watu tisa wamepandishwa kizimbani huko Zanzibar kwa tuhuma za kusababisha ajali ya meli ya Mv Spice Islander iliyotokea mwezi Septemba 2011 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200
Moja wa watuhumiwa hao ni Said Abdala aliyekuwa kepten wa meli hiyo ambaye hadi sasa hajulikani alipo lakini naye ni miongoni mwa watuhumiwa
habari zinasema kuwa kila mtuhumiwa ana tuhuma zake na watuhumiwa hao tisa walipandishwa kizimbani kila mmoja kasomewa mashtaka yake na wale ambao hawajulikani walipo nao pia wamesomewa mashtaka yao
Hata hivyo kazi kubwa inayowakabili waendesha mashtaka hao ni kukusanya ushahidi wa kutosha ili kuwatia hatiani watuhumiwa hao na kesi hiyo imeahirishwa na inatarajiwa kusikilizwa tena wiki mbili zijazo kuanzia jana
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na tume iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo inasema ujazaji wa mizigo na abiria kupita kiasi ni moja ya sababu zilizopelekea ajali hiyo kutokea