MARANGU KINUKAMORI WATER FALLS


Hii ni picha ya mfano wa mwanadada MAKINUKA ambaye zamani hizo alipata ujauzito kabla ya ndoa (mimba utotoni). Binti huyo wa Kichaga alifukuzwa nyumbani kwake na wazazi wake kutokana na kupata ujauzito huo, hivyo yeye baada ya kutimuliwa na wazazi wake aliamua kwenda hapa kwenye maporomoko hayo ya Kinukamori ili ajirushe na afariki dunia!

Wakati alipofika katika maporomoko hayo ya maji kutaka kujirusha ili afe akaona si vyema kujiua ila akaamua kurudi nyumbani kwa wazazi wake ili aombe radhi kwa kosa alilolifaya.

Lakini alipogeuka kuanza kurudi kwa wazazi kuwaomba msamaha ghafla alimuona chui akimnyatia kwa lengo la kumuua na alivyoona hana namna ya kumkwepa chui huyo basiaailiamua kujirusha katika maporomoko hayo ya maji na kufariki dunia, huo ukawa ndio mwisho wa maisha ya MAKINUKA.

Kwa mila na desturi za kichagga kwa wakati huo mtoto wa kike akipata mimba nje ya ndoa (Kabla ya kuolewa) adhabu hutolewa kwa wote (aliyempa mimba na mwenye mimba) na adhabu yao ilikuwa ni kulaliana yaani mmoja juu na mwingine chini halafu wanachomwa mti mgongoni ambao utawachoma wote hadi wafe!!!!!!!!


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo