Waziri Ulega amuumbua Luhaga Mpina

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema alishindwa kupinga maamuzi ya aliyekuwa Boss wake Luhaga Mpina baada ya Viongozi wa Wizara hiyo kwenda kupima kwa rula samaki waliopikwa kwenye mgahawa wa Bunge.


Ulega amesema hayo wakati akijibu hoja ya Mpina aliyoiibua Bungeni wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo alimtaka Waziri aeleze kanuni iliyotumika kutekeleza zoezi hilo.

“Wakati mwingine tunakaa kimya maana kukaa kimya nayo ni busara, samaki akishapikwa anapoteza shape anapoteza size sayansi ya samaki haielekei huko , samaki yule aliyepimwa na Boss wangu wa zamani (Mpina) Mheshimiwa alikuwa amekaangwa kapita katika nyuzijoto nyingi sana alipoteza uhalisia sasa alitaka wakati ule nimwambie Mzee unakosea hapa.”


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo