Bangi iliyotengenezwa kama sabuni yakamtwa Songwe

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limekamata mabunda 50 ya sigara ambayo ni paketi 500, yenye uzito wa kilo nane, ambazo zimetengenezwa kwa kutumia bangi zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Zimbabwe kuingia Tanzania.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi (ACP) Theopista Mallya, alithibitisha kukamatwa kwa dawa hizo za kulevya na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa zilikamatwa Aprili 29, mwaka huu, majira ya saa 2:45 katika mpaka wa Tunduma.

Alisema sigara hizo zenye bangi zinazoonekana katika mwonekano wa kutengenezwa kiwandani, zilikamatwa baada ya upekuzi uliofanywa kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Idara ya Forodha katika mpaka huo.

ACP Mallya alisema mzigo huo ulikuwa ukisafirishwa kwa basi la abiria la Kampuni ya Classic yenye namba za usajili za Jamhuri ya Kimodekrasia ya Kongo 6321AA25 ambalo lilikuwa likitokea Zimbabwe kwenda Dar es Salaam.

“Mabunda hayo yalikuwa yamefichwa nyuma ya kiti cha dereva yakiwa na mwonekano wa kipeto cha pakiti za sigara za kawaida zilizoandikwa Kkog Hybrid Malawi Gold,” alisema.

Kamanda Mallya alisema kutokana na tukio hilo, jeshi hilo linamshikilia kondakta wa basi hilo, Vitalian Sanga (46) mkazi wa jijini Mbeya kwa mahojiano zaidi na ushahidi ukikamilika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mallya alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu ili matukio hayo yajulikane na kuthibitiwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo